Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 09:06

Idadi ya waliofariki kutokana na ajali ya boti Nigeria yafikia 76


Raia wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya boti kwenye jimbo la Kusini Mashariki la Anambra nchini Nigeria imeongezeka na kufikia 76, rais wa nchi hiyo, Muhamadu Buhari amesema.

Boti hiyo ilizama siku ya Ijumaa huku kukiwa na mafuriko makubwa katika eneo la Ogbaru huko Anambra, kwa mujibu wa maafisa wa serikali.

Katika taarifa iliyotumwa kupitia mtandao wa Twitter Jumapili, Rais Buhari alisema kuwa mamlaka za dharura zimethibitisha idadi hiyo kubwa ya vifo.

"Mamlaka husika zinajitahidi kuopoa, kuokoa au kuwatafuta abiria wowote waliopotea," alisema Buhari.

Aliongeza kuwa ameviagiza vyombo vinavyohusika kufanyia tathmini itifaki za usalama ili kuzuia ajali zijazo.

Mkuu wa Usimamizi wa Dharura wa Jimbo la Anambra alisema kuwa watu 15 walikuwa wameokolewa kufikia Jumamosi usiku.

Anambra ni miongoni mwa majimbo 29 kati ya 36 ya Nigeria ambayo yamekumbwa na mafuriko makubwa mwaka huu.

Maji hayo yamesomba nyumba, mimea, mazao na barabara na kuathiri takriban watu nusu milioni.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG