Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 08:56

Rais Biden na mkewe Jill wafanya ziara kujionea uharibifu wa Kimbunga Ian


Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza kuhusu uharibifu uliosababishwa na kimbunga Ian na juhudi za kutoa misaada alipotembelea Fisherman's Wharf akijumuika na mkewe Jill Biden, Gavana wa Florida Ron DeSantis na mkewe huko Fort Myers Beach, Florida. Oktoba 5, 2022. REUTERS.

Rais wa Marekani Joe Biden na mke wa rais Jill Biden walitembelea Fort Myers, Florida, Jumatano, wakifanya ziara ya angani ndani ya helikopta ya rais Marine One.

Ziara hiyo ilifanyika ili kujionea uharibifu kutokana na Kimbunga Ian na kukutana na maafisa, wakazi na wamiliki wa biashara walioathiriwa na dhoruba hiyo mbaya na yenye nguvu.

Idadi ya vifo kutokana na kimbunga Ian imeongezeka na kufikia takriban watu 109, huku 105 kati ya waliofariki wakiwa Florida na wengine katika jimbo la North Carolina. Zaidi ya vifo 50 viliripotiwa katika Kaunti ya Lee ya Florida, ambayo ilibeba mzigo mkubwa wa dhoruba hiyo ilipofika ufukweni.

Biden alikutana na viongozi wa serikali na serikali za mitaa, akiwemo Gavana Mrepublican Ron DeSantis na Maseneta Marco Rubio na Rick Scott, kujadili juhudi za kurejesha hali ya kawaida.

Rais Biden amekuwa na migongano na Gavana DeSantis, mtu ambaye huenda anaweza kuwa mgombea urais wa mwaka 2024 kupitia chama cha Republikan katika masuala kuhusu uhamiaji na mengineyo na wakati huo huo Seneta Marco Rubio na Tim Scott wamekosoa vikali sera za serikali ya Biden.

Kwa sasa mahasimu hao wa kisiasa wameweka kando tofauti zao ili kuangazia juhudi za kutoa misaada baada ya kimbunga hicho kilicholikumba jimbo hilo la tatu kwa ukubwa wa idadi ya watu nchini Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG