Mzozo unaozingira swala la ni nani kiongozi halisi wa walio wengi katika bunge la Kenya, umemlazimu Spika wa bunge hilo Moses Wetangula kumteua Naibu Spika Gladys Boss kwa muda mfupi, kusimamia kamati ya kuratibu shughuli za bunge ili kusitisha usambaratishaji wa shughuli za taasisi hiyo.