Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 15:09

Mwili wa Malkia Elizabeth 11 wa Uingereza unaelekea makaburini


jeneza lililobeba mwili wa Malkia Elizabeth II linaelekea Westminster, mjini London kwa mazishi. Sept. 19, 2022.
jeneza lililobeba mwili wa Malkia Elizabeth II linaelekea Westminster, mjini London kwa mazishi. Sept. 19, 2022.

Mazishi ya kitaifa ya Malkia Elizabeth II yanafanyika Jumatatu katika eneo la kihistoria la Westminster Abbey mjini London.

Mwili wake ulikuwa umelala hapo tangu Jumatano katika ukumbi wa Westminster na maelfu ya waombolezaji walipitapembeni ya jeneza lake kutoa heshima zao.

Mamia ya wakuu wa nchi, akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden pamoja na mke wake Jill Biden, na waheshimiwa kutoka kote ulimwenguni wameingia London kuhudhuria mazishi ya Elizabeth ambayo yanatarajiwa kujaa watu kutoka pembe zote za dunia.

Zaidi ya mialiko 2,000 iliongezwa kwenye mazishi ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na mialiko kwa baadhi ya watumishi wa umma.

Malkia huyo anaripotiwa kuwa aliandika kwa mkono na kupanga baadhi ya masuala yatakayofanyika katika mazishi yake.

XS
SM
MD
LG