Vijana wengi wa Burundi wamekua wakiondoka nchini mwao na kuelekea Serbia kutafuta ajira, baada ya serikali ya Burundi na Serbia kusaini makubaliano ya kuruhusu raia wa Burundi kuingia Serbia bila visa. Lakini baadhi ya vijana hao hujipenyeza na kuingia Ubelgiji kwa kufanya safari hatarishi.