Angad Singh ambaye hutengeneza makala za televisheni za kituo cha Vice News, aliwasili India kwa ajili ya kuwasalimia ndugu na jamaa, akiwemo mama pamoja na bibi na babu yake wakati alipokataliwa kuingia India na maafisa wa idara ya uhamiaji katika uwanja wa ndege mama yake alisema.
Angad aliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Gandhi akitokea Marekani majira ya saa mbili na nusu usiku siku ya Jumatano, alimueleza mama yake Gurmeet Kaur kwa njia ya ujumbe wa simu.
Mwanahabari huyo ambaye ana uraia wa Marekani ameitembelea India mara kadhaa na amewahi kutengeneza makala siku za nyuma kuhusiasa na masuala ya maandamano ya wakulima, janga la Covid-19, na maandamano ya waislamu wa Kashmir.