Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 18:33

Matokeo ya awali yaonyesha chama tawala kinaongoza Angola


Maafisa wa wapiga kura katika vituo vyao wakati wa uchaguzi wa urais huko Luanda, Angola, Jumatano, Agosti 23,2017. (AP Photo/Bruno Fonseca).

Kura nyingi katika uchaguzi wa wabunge wa Angola zimehesabiwa na matokeo ya muda yanaonyesha kuwa chama tawala cha MPLA kiko mbele kwa asilimia 52, wakati wapinzani wao wakuu wana asilimia 42, tume ya uchaguzi ilisema Alhamisi.

Tume hiyo ilisema asilimia 86 ya kura zimehesabiwa hadi sasa, jambo ambalo lilipendekeza kwamba vuguvugu la zamani la Marxist People's Movement for the Liberation of Angola (MPLA) huenda likaongeza muda wake wa takriban miongo mitano madarakani na kumpa Rais Joao Lourenço awamu ya pili ya miaka tano.

Chama upinzani cha Angola (UNITA), kinachoongozwa na Adalberto Costa Junior, hakikujibu mara moja. UNITA ilitupilia mbali matokeo ya kwanza ya muda yaliyotangazwa na tume hiyo mapema Alhamisi kuwa si ya kutegemewa.

Mgombea makamu wa rais wa UNITA, Abel Chivu-kuvuku aliambia kituo kimoja cha cha radio cha Ureno TSF kwamba chama kinafikiria kupinga matokeo ya uchaguzi kwa sababu hayawiani na ukweli.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG