Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:51

Mikutano ya mwisho ya kampeni yafanyika Angola kuelekea uchaguzi Jumatano


Mkutano wa kampeni nchini Angola.
Mkutano wa kampeni nchini Angola.

Wagombea urais nchini Angola Jumatatu walihitimisha kampeni za mwezi mzima kabla ya uchaguzi wa Jumatano ambao huenda ukashuhudia ushindani mkali kati ya chama tawala, kilicho madarakani kwa miongo kadhaa, na upinzani unaozidi kuongeza mvuto miongoni mwa vijana.

MPLA, kinachoongozwa na João Lourenço tangu mwaka wa 2017, kimetawala nchi ya pili kwa uzalishaji mafuta barani Afrika, tangu uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975.

Lakini chama cha upinzani cha muda mrefu cha UNITA, kina nguvu zaidi kuliko hapo awali, huku hasira ikiongezeka kutokana na kushindwa kwa serikali kubadili utajiri mkubwa wa mafuta kuwa hali bora ya maisha kwa wote.

Uchaguzi wa Angola
please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:04:31 0:00

Zaidi ya Waangola milioni 14 wamejiandikisha kama wapiga kura na watamchagua rais na wabunge 220 kwa wakati mmoja, kwa kuweka alama moja kwenye karatasi ya kupigia kura.

Utafiti wa Afrobarometer mwezi Mei ulionyesha idadi ya Waangola wanaopendelea UNITA, inayoongozwa na Adalberto Costa Júnior, imeongezeka hadi 22% kutoka 13% mwaka 2019, bado pointi saba nyuma ya MPLA. Hata hivyo, wakati wa utafiti huo, aribu nusu ya wapiga kura walikuwa hawajaamua.

XS
SM
MD
LG