Baada ya serikali ya Kenya kutangaza kwamba wenye magari ni sharti wapate na kuweka vibandiko vipya vya kidijitali kwenye magari yao, maoni mseto yanaendelea kutolewa huku baadhi wakisema hatua hiyo haina umuhimu wowote huku nayo serikali ikitetea mpango huo kama njia ya kuzuia au kudhibiti uhalifu.