Moussa Faki Mahamat analaani vikali mashambulizi ya anga yanayoendelea kufanywa na Israel huko Gaza ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 30 wa Palestina, wakiwemo watoto 6, taarifa ya AU ilisema.
Kuwalenga raia na kuendelea na ukaliaji wa kimabavu unaofanywa na vikosi vya usalama vya Israel ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa, na kuleta shida katika utafutaji wa suluhu ya haki na ya kudumu”, ilisema taarifa hiyo.