Ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken katika nchi tatu za Afrika yaangazia changamoto za Rwanda na DRC. Na ziara hiyo inachangiwa na nia ya Washington ya kuzihakikishia nchi na viongozi wa Kiafrika kuwa wao ni washirika muhimu wa Marekani.