Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 13:01

Tetemeko la ardhi laua watu Ufilipino


Athari za tetemeko la ardhi la Jumatano ambalo limesababisha vifo.
Athari za tetemeko la ardhi la Jumatano ambalo limesababisha vifo.

Watu wanne wamefariki dunia Jumatano baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi kaskazini mwa Ufilipino.

Kituo cha mambo ya Jiolojia cha Marekani kinasema jimbo la Abra katika kisiwa kikuu cha Luzon kilipatwa na tetemeko la ardhi la kipimo cha 7 ambacho kiliathiri eneo la kilometa 10.

Serekali ya Ufilipino inasema takriban watu 44 wamejeruhiwa katika tuko hilo.

Serekali inasema dazeni ya majengo yalianguka ama kuharibiwa kabisa kote katika jimbo la Abra.

Picha zilizo wekwa katika ukurasa wa naibu gavana wa Abra, Joy Bernos, zinaonyesha wakazi, na wafanyakazi wakiwa wamesimama nje ya hospitali ambayo ilipata tundu kubwa upande wa mbele baada ya tetemeke.

Mtikisiko wa tetemeko ulikwenda mbali mpaka kwenye mji mkuu Manila unaopatikana kilometa 300 kusini mwa kitovu cha tetemeko hilo.

XS
SM
MD
LG