Odinga anayepeperusha bendera ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya na viongozi wa mrengo huo pamoja na wafuasi wao, walikusanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani huku Ruto, anayewania kwa tiketi ya chama cha UDA chini ya muungano wa Kenya Kwanza akijiunga na wenzake kwenye uwanja wa Nyayo.