Kufuatia Shirika la Elimu na Sayansi la Umoja wa Mataifa, UNESCO, kutenga tarehe 7 mwezi Julai kama siku ya kimataifa ya kukienzi Kiswahili, maadhimisho ya mwaka wa kwanza yalifanyika Alhamisi katika maeneo mbalimbali ulimwenguni, ambapo hafla nyingi zilifanyika kote duniani.