Viongozi wa Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi (ECOWAS) Jumapili waliondoa vikwazo vya kiuchumi na kifedha walivyoiwekea Mali, baada ya viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo kupendekeza utawala wa mpito wa miezi 24 na kutangaza sheria mpya ya uchaguzi.