Hapo awali polisi wa Nigeria wamewaokoa darzeni ya wanawake na watoto wachanga kutoka katika nyumba haramu za uzazi zinazojulikana kama "viwanda vya kuzalisha watoto" ambapo wanawake wanalazimishwa kupata uja uzito na kujifungua watoto kwa ajili ya kuuzwa kwenye soko la biashara.
msemaji wa polisi wa jimbo hilo Tochukwu Ikenga alisema Jumatano kwamba vijana hao waliokolewa kutoka hoteli ya Gally Gally siku ya Jumatatu katika jimbo la kusini mashariki la Anambra, ambako walitumiwa kama watumwa wa ngono, ukahaba na kiwanda cha watoto, .
Wasichana wanne kati ya hao walikuwa wajawazito, alisema, huku baadhi ya silaha na fedha zikipatikana kutoka hotelini hapo.