Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 23:47

Watu zaidi ya 1500 waambukizwa Monkey pox Afrika


Picha ikionyesha virusi vya monkeypox

Afrika imeorodhesha watu 1,597 wanaodhaniwa wameambukizwa na virusi vya Monkey pox tangu mwanzo wa mwaka huu ambapo 66 kati yao imethibitishwa wamefariki, kaimu mkurugenzi wa idara ya afya ya umma barani Afrika Ahmed Ogwell Ouma alisema Alhamisi.

Ugonjwa huo bado haujadhibitiwa katika bara hili, alisema, akiongeza kuwa wakati kampeni ya chanjo ya ndui inapoanza kudhibiti Monkey pox ulimwenguni inapaswa kuanza barani Afrika.

"Msimamo wetu ni kwamba chanjo ni zana muhimu na inahitaji kuanzia hapa Afrika," Ouma alisema wakati wa mkutano wa kila wiki na Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa.

Hapa... mzigo ni mkubwa, hatari iko juu na kuenea kwa kijiografia pia ni kupana," alisema.

Nchi za Afrika ambazo zimeripoti kesi zilizothibitishwa ni Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nigeria, Morocco, Ghana, Liberia na Sierra Leone, Ouma alisema.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG