Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Burundi, anaiomba serikali ya Burundi kumruhusu kuingia nchini humo, ili kutekeleza wajibu wake ipasavyo, kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika taifa hilo la Afrika Maashariki.