Kundi la la nchi saba tajiri zaidi duniani, G7, Jumapili limetangaza mradi wake kujaribu kushindana na mradi kabambe wa China wa miundombinu na ujenzi wa barabara maarufu Belt and Road Initiative, kwa kuchangisha dola bilioni 600 kwa ajili ya miradi ya kimataifa ya miundombinu katika nchi maskini.