Maelfu ya wakazi wa Bunagana na Jomba wamelazimika kwa mara nyingine kuhama makazi yao na kukimbilia nchini Uganda na wengine msituni , kufuatia mapigano mapya na makali kati ya jeshi la serikali , FARDC na waasi wa M23 karibu na mji wa Bunagana siku ya Jumapili.