Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:56

Wapiganaji wa Ukraine wamejisalimisha


Picha iliyotolewa na jeshi la Russia ikionyesha kile ambacho imedai kwamba wanajeshi wa Ukraine wamejisalimisha kutoka kiwanda cha chuma cha Azovstal karika mji wa Mariupol. May 17 2022
Picha iliyotolewa na jeshi la Russia ikionyesha kile ambacho imedai kwamba wanajeshi wa Ukraine wamejisalimisha kutoka kiwanda cha chuma cha Azovstal karika mji wa Mariupol. May 17 2022

Jeshi la Ukraine limesema kwamba linalenga kuwaondoa wanajeshi wake waliosalia katika ngome yao ya mwisho ya Mariupol, huku wapiganaji ambao wamekuwa wakizuiliwa kwa siku 82 wakianza kujisalimisha.

Mabasi yameonekana yakiondoka kutoka kiwanda kikubwa cha Azavstal, na baadhi yao yakiwasili katika mji wa Novoazovsk, unaoshikiliwa na wanajeshi wa Russia.

Wanaume waliojeruhiwa wameonekana wakiwa wamelala kwenye vitanda maalum vya kubeba wagonjwa.

Video ambayo imetolewa na wizara ya ulinzi ya Russia imeonyesha wapiganaji wakiondoka kwenye kiwanda hicho, baadhi yao wakiwa wamebebwa kwa vitanda vya wagonjwa, na wengine wakiwa wameinua mikono juu na kukaguliwa na wanajeshi wa Russia.

Russia imesema kwamba wapiganaji 256 wa Ukraine wamejisalimisha, huku 51 wakiwa wamejeruhiwa.

Ukraine imesema kwamba wanajeshi 264, wakiwemo 53 waliojeruhiwa, wameondoka kwenye kiwanda hicho cha chuma na juhudi zinaendelea kuwaondoa wale ambao bado wamo katika kiwanda hicho.

Taarifa ya mkuu wa jeshi la Ukraine imesema kwamba “oparesheni ya kijeshi katika mji wa Mariupol imefanikisha malengo yake.” Na kwamba “kamanda wa juu wa kijeshi ameamrisha wanajeshi walio Azavstal kuokoa maisha ….. waliopigana kulinda Mariupol ni mashujaa.”

Kujisalimisha kwa wanajeshi hao inaonekana kuwa ishara ya kumalizika kwa mapigano makali ya Mariupol, ambapo Ukraine inaamini kwamba maelfu ya watu wameuawa kufuatia mashambulizi ya miezi kadhaa ya wanajeshi wa Russia.

Mji huo umehairbiwa vibaya, na Russia imejitangazia ushindi kwa kuuteka na hivyo kuwezesha Moscow kudhibithi kabisa pwani ya Azov na sehemu za mashariki na kusini mwa Ukraine, ukubwa wa Ugiriki.

Hata hivyo, Russia imeshindwa kabisa kudhibithi sehemu zingine, wanajeshi wake walio katika mji wa Kharkiv, ulio kaskazini mashariki, wakiondoka kwa kiwango kikubwa tangu walipofurushwa kutoka sehemu za kaskazini na sehemu zilizo karibu na Kyiv, mwishoni mwa mwezi March.

XS
SM
MD
LG