Kufuatia hotuba ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni jana Jumapili, ambapo alisema hakuna uwezekano wowote wa punguza kodi, aili kupunguza athari za kupanda kwa gharama ya maisha, baadhi ya vijana nchini humo wanasema hawana matumaini ya kuimarisha hali yao ya maisha katika mazingira ya sasa.