Baadhi ya vijana kaskazini mwa Kenya wameachana na ujambazi na kutafuta njia mbadala za kujipatia riziki. Zaidi ya wanaume 500 kutoka jamii ya Wasamburu wanaojulikana kitamaduni kama morani, wamejiandikisha katika mafunzo ya ufundi, kama vile useramala.