Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:09

Biden kushiriki hafla ya chama cha waandishi wa habari wa White House


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Jumamosi jioni atarejelea utamaduni wa Washington wa kuhutubia waandishi wa habari wanaowakilisha mashirika mbalimbali ya habari katika ikulu kwenye dhifa ya chakula cha jioni.

Kama mgeni wa Chama cha Waandishi wa habari katika ikulu ya White House, Biden atakuwa rais wa kwanza kuzungumza katika hafla hiyo ya kila mwaka tangu mwaka wa 2016.

Baada ya kuahirishwa kwa miaka miwili kwa sababu ya janga la COVID-19, na kususiwa na Donald Trump wakati wa urais wake, hafla hiyo inarudi kwa shauku mwaka huu, ikijumuisha hotuba ya mcheshi, Trevor Noah.

Zaidi ya karamu 20 zinazohusiana na hafla hiyo zinaandaliwa kote mjini Washington DC, na maafisa kadhaa wakuu wa utawala watahudhuria pamoja na watu mashuhuri kutoka ulimwengu wa burudani.

Hata hivyo, kuongezeka kwa hivi karibuni kwa visa vya COVID-19 mjini Washington kumesababisha wasiwasi na kupelekea White House kuchukua hatua za tahadhari.

Waandalizi wanahitaji kila mhudhuriaji kupimwa virusi vya Corona, na baadhi ya maafisa wakuu, akiwemo mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza Dk. Anthony Fauci, wamesema hawatahudhuria.

Chama cha Waandishi wa Habari cha White House kilianzishwa mwaka wa 1914 na kimekuwa kikiandaa chakula cha jioni karibu kila mwaka tangu kile cha kwanza mnamo 1921 kusherehekea wanahabari wanaoripoti habari za urais na kuchangisha pesa za ufadhili wa masomo.

XS
SM
MD
LG