Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 15:16

Waziri wa ulinzi wa Marekani asema Ukraine inaweza kushinda vita vya Russia


Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akizungumza wakati wa mkutano kuhusu usalama nchini Ukraine uliofanyika Ujerumani April 26 2022. PICHA: AFP
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akizungumza wakati wa mkutano kuhusu usalama nchini Ukraine uliofanyika Ujerumani April 26 2022. PICHA: AFP

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ameelezea Imani yake kwamba Ukraine inaweza kushinda vita dhidi ya Russia, ambavyo vimechukua muda wa miezi miwili.

Lloyd alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mazungumzo kuhusu ulinzi, yanayohusisha zaidi ya nchi 40.

Austin amesema kwamba hatua ya Ukraine kupambana na Russia imetoa motisha kwa ulimwengu, huku akilaani uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Amesema kwamba Ukraine inaamini kwamba inaweza kushinda namna kila mtu anavyoamini.

Wakati huo huo, Ujerumani imeidhinisha rasmi hatua ya kupelekea mfumo wa kuzuia mashambulizi ya ndege kwa Ukraine.

Mbunge wa ngazi ya juu kutoka muungano wa vyama vya kisiasa nchini Ujerumani Johannes Vogel, amethibitisha taarifa hizo.

Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amekosolewa ndani na nje ya Ujerumani kwa kukosa kuipatika Ukraine silaha nzito nzito, lakini ameahidi kutoa silaha hizo za ulinzi.

XS
SM
MD
LG