Guterres alisafiri hadi kambi ya Ouallam nchini Niger katika siku ya nne ya ziara yake ya Afrika magharibi iliyocheleweshwa na mzozo wa Ukraine. Alikutana na darzeni kadhaa za watu waliokoseshwa makazi na wakimbizi kutoka Niger, Mali na Burkina Faso katika uwanja wa shule uliopo kwenye kambi hiyo