Kulingana na gazeti la The Citizen la nchini Tanzania, ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali, ambayo ilitolewa jumanne katika makao makuu ya serikali Dodoma, jumla ya wanaume 731 walihusika na ulaghai huo.
“Madai ya malipo yasiyo ya kweli, yaliasilishwa na hospitali mbalimbali na jumla ya shilingi za Tanzania 14,409,200 (dola 6,211) zililipwa.” Imesema ripoti ya CAG, ikiongezea kwamba “kulikuwa a madai 56 yaliyoonyesha kwamba wanaume walijifungua kwa njia ya upasuaji au ya kawaida.”
Kulingana na mkaguzi mkuu wa serikali, watu 444 walifanyiwa ukaguzi wa damu, zaidi ya mara moja kwa siku moja.
“wengine walifanyiwa ukaguzi wa damu zaidi ya mara 30 katika hospitali moja.”
Ripoti inaendelea kusema kwamba kuna watu ambao walitumia bima ya afya ya taifa kupokea miwani zaidi ya mara mbili kwa mwaka, wakati sheria inaruhusu mtu kupokea miwani mara moja kwa mwaka.
Kati yam waka 2020 na 2021, jumla ya watu 7,556 walidai shilingi za Tanzania milioni 69.1 (dola 29,785) na kwamba majina ya waliofaidhika na pesa hizo hayalingani na wenye kadi za bima.