Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 15:55

HRW inaelezea wasiwasi kuhusu kuteswa wafungwa nchini Uganda


Ripoti ya Human Rights Watch inaelezea Uganda inatumia vituo vya siri kuwakandamiza wapinzani
Ripoti ya Human Rights Watch inaelezea Uganda inatumia vituo vya siri kuwakandamiza wapinzani

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Ulaya siku ya Jumatano alielezea wasiwasi wake kuhusu kuteswa kwa wafungwa nchini Uganda na ukiukwaji mwingine wa haki akimtaka Rais Yoweri Museveni kuhakikisha kuna hatua za kukomesha vitendo hivyo na sio maneno pekee.

Eamon Gilmore alisema ameelezea wasi-wasi wa umoja huo, katika mazungumzo na kiongozi huyo mkongwe wa Uganda na maafisa wengine wakati wa ziara yake mjini kampala. Ziara yake inajiri wiki mbili baada ya Human Rights Watch kutoa ripoti ikisema kuwa serikali inatumia vituo vya siri vinavyojulikana kama nyumba salama kuwakamata wapinzani na kuwatesa mateka.

Alisema tulielezea wasiwasi wetu kuhusu watu kuteswa wakiwa kizuizini. Ni muhimu kukomesha tabia hiyo pia ni muhimu kuwaangazia wale ambao wamehusika na mateso Gilmore alisema katika mkutano na wanahabari.

Pia tulizungumzia suala la kupotea kwa kulazimishwa, mauaji holela, suala la kile kinachojulikana kama “nyumba salama”, aliongeza akisema kwamba ripoti hizo zinahitaji kuchunguzwa na wale wenye hatia wawajibishwe.

XS
SM
MD
LG