Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 19, 2025 Local time: 00:57

Miaka 25 jela ya Rusesabagina; waendesha mashtaka wadai haitoshi


Paul Rusesabagina akiwa katika mahakama moja mjini Kigali huko Rwanda
Paul Rusesabagina akiwa katika mahakama moja mjini Kigali huko Rwanda

Raia mmoja wa Rwanda aliyeorodheshwa kama shujaa katika filamu ya Hotel Rwanda hapaswi kuongezewa kifungo chake cha miaka 25 hadi kifungo cha maisha jela mahakama ya Rwanda iliamua Jumatatu.

Paul Rusesabagina alipatikana na hatia mwezi Septemba kwa mashtaka manane ya ugaidi kwa jukumu lake katika kundi moja linalompinga Rais Paul kagame. Alisema kwamba yeye alikuwa kiongozi wa chama cha Rwanda Movement for Democratic Change lakini hakuwa na jukumu lolote katika mrengo wa kijeshi wa kundi hilo la National Liberation Front ambalo limefanya mashambulizi.

Alikataa kushiriki katika kesi hiyo ya Septemba akiiita udanganyifu na hakuwepo katika uamuzi wa Jumatatu. Waendesha mashtaka waliitaja hukumu hiyo ya miaka 25 kuwa nyepesi mno.

Familia yake inafanya kampeni ya kuomba kuachiliwa kwake, ikisema Rusesabagina ni mgonjwa. Rusesabagina aliwaokoa takribani watu 1,200 kwa kuwahifadhi katika hoteli wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo zaidi ya watu laki nane waliuawa.

XS
SM
MD
LG