Baraza la seneti la Marekani limemuidhinisha Jaji Ketanji Brown Jackson kuwa jaji wa mahakama ya juu ya Marekani kwa kura 53 dhidi ya 47. Baraza la Seneti lilipiga kura Alhamis na kumfanya Jackson mwenye umri wa miaka 51 kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuhudumu katika mahakama ya juu Marekani