Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:28

Vikosi vya usalama Sudan vimesababisha kifo na maafa kwa waandamanaji


Waandamanaji Sudan wanaendelea kuandamana wakipinga jeshi kuchukua madaraka
Waandamanaji Sudan wanaendelea kuandamana wakipinga jeshi kuchukua madaraka

Vikosi vya usalama vya Sudan vilimpiga risasi na kumuua kijana mmoja siku ya Jumatatu wakati wa msako mkali dhidi ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka jana madaktari walisema.

Sudan imekumbwa na machafuko makubwa tangu mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan ambayo yamesababisha maandamano ya mara kwa mara. Babiker al-Rashid mwenye umri wa miaka 17 aliuawa huko Omdurman baada ya kupigwa risasi ya moja kwa moja kifuani na mamlaka ya mapinduzi ilisema taarifa ya kamati kuu ya madaktari wa Sudan. Kifo chake kinafikisha idadi ya watu 89 waliouawa katika harakati za kupinga mapinduzi kamati hiyo ilisema.

Mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 25 yalivuruga makubaliano dhaifu ya kushirikiana madaraka kati ya jeshi na raia yaliyojadiliwa baada ya kuondolewa kwa kiongozi wa muda mrefu nchini Sudan Omar al-Bashir hapo mwaka 2019. Maandamano ya Jumatatu yalifanyika haswa katika mji mkuu Khartoum na miji jirani ya Omdurman na kaskazini mwa Khartoum.

Vikosi vya usalama vilifyatua gesi ya kutoa machozi ili kuzima maandamano hayo kwa mujibu wa walioshuhudia. Maandamano ya Jumatatu yalikuja huku Marekani ikisema kwamba imeweka vikwazo kwa Central Reserve Police (CRP) nchini Sudan kutokana na matumizi yake ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia kulingana na waziri wa fedha Brian Nelson.

Chini ya vikwazo hivyo mali yoyote ya CRP nchini Marekani itazuiliwa Viongozi wa Sudan wamekanusha mara kwa mara kuwafyatulia risasi waandamanaji.

XS
SM
MD
LG