Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 19:26

Watu 52 wauawa kaskazini mashariki mwa DRC.


 Wanajeshi kutoka Morocco wa kikosi cha Umoja wa mataifa huko DRC( Monusco) wakipiga doria katika wilaya ya Djugu, mkoa wa Ituri. Machi 13, 2019.
Wanajeshi kutoka Morocco wa kikosi cha Umoja wa mataifa huko DRC( Monusco) wakipiga doria katika wilaya ya Djugu, mkoa wa Ituri. Machi 13, 2019.

Zaidi ya watu 50 waliuawa kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaodhaniwa kuwa wa kundi la ADF, chanzo kutoka eneo hilo kilisema Jumatatu.

Christophe Munyanderu anayefanya kazi na shirika lisilokuwa na kiserikali linalotetea haki za binadamu katika mkoa wa Ituri, alisema mauaji hayo ni kufuatia mashambulizi kwenye vijiji kadhaa.

Alisema waasi wa ADF walishambulia vijiji vinne Jumapili na kuua watu 19, katika wilaya ya Irumu.

Jana Jumatatu, waasi hao walishambulia vijiji vingine viwili na kuua watu 33, ameongeza Munyanderu.

Alisema jumla ya watu 52 waliuawa Jumapili na Jumatatu.

Mauaji hayo yanafuatia mauaji ya watu wengine 30 yaliofanywa na waasi wanaoshukiwa kuwa wa kundi la ADF huko Kivu kaskazini mwishoni mwa wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG