Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:27

Luteni Jenerali Dagalo wa Sudan yupo Russia kwa mazungumzo na Putin


Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, kutoka serikali ya kijeshi ya Sudan
Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, kutoka serikali ya kijeshi ya Sudan

Serikali ya kijeshi ya Sudan inatafuta ufadhili kutoka Russia kufuatia nchi za Magharibi kusitisha misaada ya kifedha kwa Khartoum.

Luteni Jenerali wa Sudan Mohamed Hamdan Dagalo anayejulikana pia kama Hemedti alikuwa mjini Moscow siku ya Alhamis kujadili uhusiano wa nchi hizo mbili na Russia muda mfupi wakati Rais wa Russia Vladmir Putin alipofanya uvamizi kwa Ukraine na hivyo kuzua shutuma za kimataifa.

Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi, Samah Salman pamoja na jumuiya ya wasomi wa Sudan waliosomea Marekani wanasema ziara ya Hemedti mjini Moscow lazima iangaliwe katika muktadha wa matatizo ya kiuchumi ya Sudan ambayo yalizidi kuwa mabaya zaidi pale Marekani na nchi nyingine za magharibi zilipositisha msaada wa kifedha na kutengua uamuzi wa awali wa kufuta sehemu kubwa ya deni la Sudan.

Tangu wakati huo, sarafu ya Sudan imezidi kushuka dhidi ya dola ya Marekani wakati mfumuko wa bei wa nchi hiyo ukibaki kuwa juu zaidi duniani.

XS
SM
MD
LG