Taarifa ya serikali inasema kwamba “ Serikali ya Mali inafahamisha wanainchi wa Mali na jumuia ya kimataifa kwamba leo, balozi wa Ufaransa mjini Bamako Joel Meyer, aliitishwa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na kwamba amejulishwa kuhusu uamuzi wa serikali ambayo imemtaka kuondoka nchini ndani ya saa 72”.
Viongozi wa Mali wameeleza kwamba uamzi huo umechukuliwa kutokana na kauli za chuki za hivi karibuni za maafisa wa Ufaransa dhidi ya utawala wa Mali.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulizorota tangu pale maafisa wa jeshi walichukuwa madaraka mwezi Agosti mwaka wa 2020 na kuliongoza taifa hilo ambalo linakumbwa na mzozo mkubwa wa kisiasa na usalama tangu mwaka wa 2012.
Facebook Forum