Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:55

Rais wa Malawi awafuta kazi mawaziri wote


Rais wa Malawi Lazarus Chakwera.
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera.

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amelifuta kazi baraza lote la mawaziri kutokana na madai ya ufisadi.

Katika hotuba kwa taifa kwa njia ya televisheni, Chakwera ameapa kukabiliana na aina zote za ukiukaji wa sheria unaofanywa na maafisa wa umma.

Amesema kwamba atatangaza baraza jipya katika muda wa siku mbili zijazo.

Mawaziri watatu wanakabiliwa na mashtaka mahakamani, akiwemo Waziri wa ardhi aliyekamatwa mwezi uliopita kwa madai ya kupokea hongo.

Waziri wa kazi anashutumiwa kwa kutumia vibaya pesa zilizo tengwa kukabiliana na janga la virusi vya Corona, huku Waziri wa nishati akishutumiwa kwa kuingia mikataba ya kijanja kuhusu mafuta.

Mawaziri wote waliotajwa wamekana madai hayo.

Chakwera alichaguliwa mwaka 2020 kutokana na ahadi yake ya kupambana na ufisadi.

Makundi yenye nguvu sana katika makanisa, yalimueleza wiki iliyopita kwamba hakuwa anachukua hatua za kutosha kupambana na ufisadi.

XS
SM
MD
LG