Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 08:07

Amazon yatishia kujiondoa kwenye makubaliano ya ujenzi wa makao yake makuu huko Afrika Kusini.


Makao makuu mapya ya Amazon, Pittsburgh, Pennsylvania. Picha ya AP
Makao makuu mapya ya Amazon, Pittsburgh, Pennsylvania. Picha ya AP

Kampuni kubwa ya hapa Marekani inayofanya biashara ya mtandaoni ya reja reja Amazon, inaweza kujiondoa katika makubaliano ya kujenga makao yake makuu ya kikanda mjini Cape Town Afrika Kusini, ikiwa pingamizi la wanaharakati wa haki za watu wa asili itaruhusiwa kuendelea.

Mahakama imesikiliza pingamizi hiyo leo Alhamisi.

Ujenzi tayari unaendelea kwa ajili ya makao makuu hayo ya Amazon barani Afrika, ambao utagharimu dola milioni 262, kwenye ardhi ambayo jamii ya Wakhoisan huichukulia kuwa takatifu, kama kituo cha upinzani wao wa miaka ya awali dhidi ya wakoloni wa Ulaya mnamo mwaka wa 1510.

Makundi mengi ya Wakhoisan yaliunga mkono mradi huo baada ya kukubialana na waandaji wa mradi huo kuwajengea kituo cha urithi , utamaduni na vyombo vya habari, ambacho kitasimamiwa na makundi ya watu wa asili.

Lakini baraza la kijadi la Wakhoisan na shirika lingine la kitongoji waliiomba mahakama kuu ya Western Cape kusitisha ujenzi huo.

XS
SM
MD
LG