Televisheni ya Brazil Globo imeonyesha picha za Bolsanaro akishuka kwenye ndege ya rais baada ya kutua mjini Sao Paulo, kisha akapelekwa kwenye hospitali ya Vila Nova Star, Globo imesema.
Bolsanaro alilazwa hospitali mara kadhaa tangu alipochomwa kisu wakati wa kampeni ya urais mwaka 2018.
Julai 2021, alipelekwa hospitali hiyo ya Vila Nova Star kwa sababu ya kuziba kwa utumbo.