Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:52

Rais wa zamani wa Korea kusini Park, aachiliwa huru kutoka jela kwa msamaha wa rais


FILE - Rais wa zamani wa Korea kusini Park Geun-hye akifika mahakamani mjini Seoul, Oktoba 10, 2017. Picha ya AP
FILE - Rais wa zamani wa Korea kusini Park Geun-hye akifika mahakamani mjini Seoul, Oktoba 10, 2017. Picha ya AP

Rais wa zamani wa Korea kusini Park Geun-hye ameachiliwa huru kutoka jela leo Ijumaa karibu miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi, na hivyo kuzusha mjadala iwapo atakuwa na jukumu lolote kabla ya uchaguzi wa rais wa mwezi Machi.

Park, mwenye umri wa miaka 69, alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo aliyechaguliwa kidemokrasia na kuondolewa madarakani, wakati mahakama ya katiba ilipokubaliana na kura ya bunge mwaka 2017 ya kumshtaki kumuondoa madarakani kwa kashfa ambayo ilisababisha kufungwa kwa wakuu wa makumpuni mawili makubwa ya Samsung na Lotte.

Mahakama ya juu ya Korea kusini mwezi Januari ilikubaliana na kifungo cha miaka 20 jela kilichotolewa, baada ya Park kukutwa na hatia ya kushirikiana na rafiki yake ambaye yuko pia jela, kwa kupokea ma bilioni ya pesa kutoka kwenye makampuni hayo, pesa hizo zilikuwa za kuifadhili familia ya rafiki yake na mashirika yasiyotafuta faida.

Rais Moon Jae-in alitoa msamaha maalumu kwa Park wiki iliyopita, akielezea kuzorota kwa hali yake ya afya na kuelezea matumaini yake ya kusahau historia mbaya ya zamani na kuimarisha umoja wa kitaifa.

Maafisa wa wizara ya sheria waliwasilisha msamaha huo kwa Park usiku wa manane siku ya alhamisi katika hospitali ambako amekuwa kwa mwezi mmoja, shirika la habari la Yonhap limeripoti.

XS
SM
MD
LG