Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 21:03

Mazungumzo kuhusu mkataba wa nuclear wa Iran kuanza tena Jumatatu


Wajumbe katika mazungumzo ya mkataba wa nuclear
Wajumbe katika mazungumzo ya mkataba wa nuclear

Mazungumzo ya kunusuru mkataba wa Iran kuhusu y nuclear yataanza tena Jumatatu wiki ijao.

Ofisi ya mambo ya nje ya umoja wa ulaya imesema kwamba mkutano huo utahudhuriwa na wawakilishi kutoka China, Ufaransa, Ujerumani, Russia, Uingereza na Iran.

Washiriki wataendelea na mazungumzo kuhusu uwezekano wa Marekani kurudi katika mkataba wa nuclear na Iran.

Mazungumzo pia yataangazia pia namna ya kuhakikisha kwamba makubaliano yatatekelezwa kikamilifu na kila upande.

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Russia Mikhail Ulyanov, amesema kwamba washiriki katika mazungumzo hayo wanalenga kuhakikisha kwamba mkataba huo unarudishwa haraka iwezekanavo.

XS
SM
MD
LG