Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 02:04

Vikosi vya Ethiopia vyasema vimesafisha himaya za TPLF


Serekali ya Ethiopia, Jumanne imesema jeshi lake lilikuwa likisafisha himaya za vikosi vya Tigray katika mikoa ya kaskazini ya Amhara na Afar.

Habari hizo zinakinzana na taarifa za Wa-Tigray kwamba vikosi vyake vilijiondoa vyenyewe ili kuweka mazingira mazuri ya kuleta amani.

Maelfu ya raia wameuwawa kutokana na vita vya miezi 13 huku wengine 400,000 wakikabiliwa na hali ya ukame katika eneo la Tigray, na watu milioni 9.4 wakihitaji msaada wa chakula kote kaskazini mwa Ethiopia.

TPLF chama kinacho tawala Tigray ambacho kipo vitani na serekali, kilitangaza kujitoa katika mikoa ya karibu ya Amhara na Afar Jumatatu.

Msemaji wa serekali Billene Seyoum aliwaeleza wanahabari katika mkutano kwamba kama ilivyo shuhudiwa katika wiki za hivi karibuni, vikosi vya taifa pamoja na vikosi shirika kutoka mikoa ya Afar na Amhara vimetwaa miji iliyokuwa inashikiliwa na TPLF.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG