Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 14:20

Malaysia: mafuriko yasababisha uharibifu mkubwa katika majimbo 6


Watu waliokwama ndani ya magari yao kutokana na mafuriko katika mji wa Shan Alam, karibu na mji wa Kuala Lumpur, Malaysia, Dec 20, 2021
Watu waliokwama ndani ya magari yao kutokana na mafuriko katika mji wa Shan Alam, karibu na mji wa Kuala Lumpur, Malaysia, Dec 20, 2021

Maelfu ya watu wamekosesehwa makazi kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Malaysia.

Hali ni mbaya katika majimbo sita ambapo karibu watu 21,000 wameondolewa makwao na kuwekwa katika makao ya muda.

Waziri mkuu Ismail Sabri Yaakob, amewaambia waandishi wa habari kwamba kiwango cha mvua iliyoanza kunyesha ijumaa, ni sawa na kiwango cha mvua ya kawaida inayonyesha kwa mwezi mzima.

Waziri mkuu ameahidi kutoa msaada kwa waathirika haraka iwezekanavyo. Ametenga dola milioni 23.7 kukarabati nyumba na miundo mbnu iliyoharibiwa kutokana na mafuriko hayo.

Juhudi za uokoaji zinaendelea kwa wale waliokwama kwenye magari na nje ya nyumba zao.

XS
SM
MD
LG