Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 04:25

Polisi wapiga kambi kwa Bobi Wine, Museveni aongoza kampeni katika uchaguzi mdogo


Kiongozi wa upinzani Uganda Bobi Wine akihutubia waandishi wa habari, Kampala.
Kiongozi wa upinzani Uganda Bobi Wine akihutubia waandishi wa habari, Kampala.

Polisi wameizingira nyumba  ya kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayejulikana sana kama Bobi Wine ili kumzuia kutoka na kufanya kampeni katika uchaguzi mdogo katika wilaya ya Kaunga, kilomita 55 kaskazini mashariki mwa Kampala.

Bobi wine ameandika ujumbe wa twiter, unaoambatana na picha, kuonyesha namna polisi wamepiga kambi nyumbani kwake.

Bobi Wine alikuwa amepanga kumfanyia kampeni mgombea wa chama chake cha NUP kujaza nafasi ya mwenyekiti wa wilaya.

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa wilayani Kaunga kumfanyia kampeni mgombea wa chama kinachotawala cha National resistance movement NRM.

Uchaguzi utafanyika alhamisi wiki hii.

Vyombo vya habari vya Uganda vimeripoti kwamba idadi kubwa ya polisi na wanajeshi wanashika doria wilayani Kayunga wakati kampeni zikiendelea.

Kayunga ilikuwa ngome ya kisiasa ya chama kinachotawala hadi viongozi kadhaa walipochaguliwa kwa tiketi ya chama cha upinzani katika uchaguzi mkuu uliopita.

Uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia kifo cha mwenyekiti aliyechaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

XS
SM
MD
LG