Serikali ya Ghana imesema kwamba wasafiri wote wanaoingia nchini humo kuanzia saa sita usiku jumapili hii, wanastahili kuwa wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya Corona.
Wizara ya huduma za afya imesema kwamba raia wa Ghana wanaopanga kurudi nchini humo wanalazimishwa kupokea chanjo wanaporejea nchini humo.
Raia wote wa Ghana wanaosafiri nje ya nchi lazima wawe wamepata chanjo hiyo dhidi ya Corona.
Amri hiyo ni sehemu ya mikakati ya kukabiliana na maambukizi ya aina mpya ya virusi vya Corona, Omicron.
Wizara ya afya ya Ghana imesema kwamba watu wanaogunduliwa kuambukizwa Omicron nchini humo, ni wasafiri wanaowasili nchini kupitia uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa wa Accra, na wengi waoa hawajapata chanjo.
Watu 130,000 wameripotiwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Ghana. Watu 1,200 wamefariki dunia.