Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 06:31

Wanajeshi wa Uganda wahukumiwa kwa kuua waandamanaji


Wanajeshi wa Uganda wakishika doria karibu na nyumbani kwa aliyekuwa mgombea wa urais Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, Magere, Uganda, Jan. 18, 2021.
Wanajeshi wa Uganda wakishika doria karibu na nyumbani kwa aliyekuwa mgombea wa urais Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, Magere, Uganda, Jan. 18, 2021.

Mahakama ya kijeshi nchini Uganda, imewahukumu wanajeshi watatu kwa kuwaua watu watatu wakati wa maandamano ya mwaka uliopita.

Maandamano yalianza baada ya kukamatwa kwa aliyekuwa mgombea wa urais Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, akiwa kwenye kampeni.

Mwanajeshi mmoja amehukumiwa maisha gerezani kwa kumuua fundi wa magari Grace Walungama, aliyedaiwa kuwa mmoja wa watu waliokuwa wakiandamana. Mwanajeshi huyo pia alimuua mwenzake aliyekataa kusaidia kuwakamata waandamanaji.
mwanajeshi wa pili amehukumiwa miaka 35 gerezani kwa kumuua Ibrahim Kirevu, aliyekuwa amemkamata na alihitajika kumpeleka katika kizuizi cha polisi lakini akamuua kwa kumpiga risasi.

Wanajeshi hao ni wa kwanza kufungwa jela kuhusiana na mauaji hayo yaliyotokea mwishoni mwa mwaka uliopita.

Zaidi ya watu 50 waliuawa.

Polisi walidai kwamba Bobi Wine alikuwa amekamatwa ili kumzuia kukusanya wafuasi wake wakati wa kampeni ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona.

XS
SM
MD
LG