Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 13:55

Mswada wa umiliki wa ardhi waanguka katika bunge la Afrika kusini


Afisa wa polisi akipandisha bendera nje ya bunge la Afrika kusini mjini Cape Town, Afrika kusini, Nov. 25, 2020.
Afisa wa polisi akipandisha bendera nje ya bunge la Afrika kusini mjini Cape Town, Afrika kusini, Nov. 25, 2020.

Bunge la Afrika kusini limepinga pendekezo la serikali la kutaka kufanya marekebisho ya katiba ili kuweza kuchukua ardhi kutoka kwa wamiliki wazungu bila kutoa fidia.

Katika kikao cha jana jumanne, mbunge wa chama kinachotawala cha African national congress ANC, Mathole Motshekga, anayeoongoza kamati iliyoandika mswada huo, amesema kwamba bunge lilikuwa na fursa ya kutatua uhalifu dhidi ya haki ya wa-Afrika na unyakuzi wa ardhi.

Vyama vikuu vya upinzani - EFF na Democratic alliance, havikuunga mkono mswada huo.

Kiongozi wa EFF Julius Malema amesema mswada huo ulishindwa kwa sababu chama cha ANC haikupendekeza ilipaji fidia, jambo ambalo chama cha EFF kilihitaji lizingatiwe sana.

Chama cha Democratic alliance nacho kimesema kwamba mswada huo utailetea Afrika kusini matatizo.

XS
SM
MD
LG