Ousainou Darboe, aliyemaliza wa pili katika uchaguzi mkuu wa urais nchini Gambia, amesema kwamba anapanga kupinga rasmi mahakamani matokeo ya uchaguzi huo ambao Adama Barrow alishinda kwa asilimia 53.
Darboe ni mmoja wa wagombea watatu waliotilia mashaka matokeo ya uchaguzi huo lakini mmoja wao – Essa Mbaye Fall, amemtumia ujumbe wa pongezi Adama Barrow kwa ushindi wake, akitoa wito kwa wafuasi wake kuwa watulivu.
Waangalizi wa uchaguzi huo kutoka umoja wa Afrika wamesema kwamba uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki.