Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 16:02

Mataifa sita ikiwemo Marekani yana wasiwasi na ukamatwaji watu Ethiopia.


Mataifa sita ikijumuisha Marekani, yameelezea wasiwasi mkubwa walionao kufuatia taarifa kwamba serekali ya Ethiopia inafanya ukamataji mkubwa wa watu kwa kuangalia makabila na kutowafungulia mashitaka.

Novemba 2 serekali ya Ethiopia ilitangaza hali ya tahadhari wakati wapiganaji wa Tigray walipokuwa wakielekea katika mji mkuu wa Addis Ababa, baada ya kuwa vitani kwa mwaka mmoja.

Serekali ya Ethiopia inasema watu wanaoshikiliwa wanashutumiwa kwa kuwasaidia wapiganaji wa Tigray.

Lakini makundi ya haki za binadamu ikijumuisha idara ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Amnesty International na tume ya Ethiopia ya haki za binadamu zimeripoti kufanyika ukamataji.

Inaelezwa matendo hayo yanafanyika kwa kiwango kikubwa kwa watu wa kabila la Tigray, ikijumuisha wachungaji wa Orthodox, wazee na mama wanaolea watoto.

XS
SM
MD
LG