Waziri mkuu wa Sudan aliyerudishwa madarakani Abdalla Hamdok ameamrisha kusitishwa zowezi la kufutwa kazi maafisa wa serikali na kutaka ukaguzi ufanyike kuhusu uteuzi na ufutaji kazi wa maafisa kwenye nyadhifa muhimu uliofanywa na jeshi.
Baada ya kuchukuwa madaraka tarehe 25 Oktoba, Jenerali Abdel Fattah Burhan aliwateuwa maafisa wa zamani wa kiongozi aliyepinduliwa Omar al Bashir kwenye nyadhifa muhimu katika uongozi wa serikali na kuvunja baadhi ya idara muhimu za serikali pamoja na wakuu wa kampuni za umaa, wakuu wa vyombo vya habari hadi wakuu wa mikoa mingi.
Aidha, uteuzi na ufutaji kazi wote ambao umefanyika chini ya kipindi kilichopita, utafanyiwa uchunguzi, tathimini na uhakiki, sekretariati ya serikali ya Sudan imesema.