Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 04:51

Makundi 9 ya wapiganaji yaungana dhidi ya serikali ya Ethiopia


Mpiganaji wa kundi la Afar akiwa Bisober, Tigray, Ethiopia
Mpiganaji wa kundi la Afar akiwa Bisober, Tigray, Ethiopia

Makundi 9 yanayopiga vita serikali ya Ethiopia, yametangaza kuunda muungano hii leo ili kulazimisha mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Hatua hiyo inaongeza shinkizo dhidi ya Waziri mkuu Abiy Ahmed, wakati makundi ya wapiganaji yakiendelea kukaribia mji mkuu wa Addis Ababa.

Makundi kadhaa yamejihami kwa silaha japo haijabainika iwapo makundi yote yanayopinga serikali yana silaha.

Makundi ya wapiganaji wa Oromo na lile linalodai kupigania demokrasia la Agaw, yameambia shirika la habari la Reuters kwamba muungano huo unaojumulisha wapiganaji wa Tigray, ni halali.

Wapiganaji wa Tigray wamekuwa wakipigana na serikali kwa mwaka mmoja sasa katika vita ambavyo vimeua maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni mbili kutotoka makwao.

Mataifa ya Afrika na ya magharibi yamekuwa yakitaka mapigano kusitishwa mara moja nchini Ethiopia, baada ya wapiganaji wa Tigray kusema kwamba wanaelekea kudhibithi mji mkuu wa Addis Ababa wiki hii.

Wapiganaji wametangaza kudhibithi mji wa Kemise, kilomita 325 kutoka Addis, lakini serikali imefutilia mbali madai hayo na kusema kwamba wapiganaji wanatoa habari za uongo kuhusu walipofikia.

XS
SM
MD
LG