Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameitisha mkutano wa viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki Novemba 16 ili kujadili mzozo wa Ethiopia, afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Uganda alisema leo Alhamisi.
Okello Oryem, waziri wa mambo ya nje wa Uganda aliiambia Reuters kwamba “Rais Museveni anawasiliana na Waziri Mkuu Abiy kuhusu hali inavyoendelea nchini Ethiopia na ameelezea wasiwasi wake kutokana na kukataa kwa kundi la Tigray kushiriki katika mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano